WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA FOLENI (QMS)
Posted on: December 29th, 2023Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa foleni Queue Management System (QMS).
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku ya jana 28/12/2023 na kuhudhuriwa na watumishi kutoka idara na vitengo mbalimbali vya Hospitali. Mafunzo hayo yalitolewa na kampuni ya Nunuget ambao ni wabunifu na wasambazaji mfumo wa usimamizi wa foleni Queue Management System (QMS).
Lengo kubwa la mfumo wa usimamizi wa foleni ni kupunguza foleni kwa wagonjwa na mgonjwa kujua mahali sahihi pakwenda kupata huduma za kimatibabu ndani ya hospitali.