Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE - MARA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA PEPMIS.

Posted on: January 22nd, 2024

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya leo 22/01/2024 wamepata mafunzo ya mfumo wa kieletroniki wa usimamizi wa utendaji kazi (PEPMIS).

Lengo kuu la mfumo huo ni kuwawezesha viongozi kusimamia utendaji kazi wa watumishi na kupima utendaji kazi kwa taasisi mbalimbali za umma.

Mfumo huo ni mbadala wa mfumo uliokuwa ukitumika hapo mwanzo wa OPRAS, Mafunzo haya yametolewa na maafisa kutoka ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora.