Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WATOA ZAWADI WODI LA WATOTO WACHANGA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE-MARA

Posted on: March 8th, 2024

Katika kuendelea kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa Machi 08 ya kila Mwaka ulimwenguni.

Siku ya leo Machi 09, 2024 Waaandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Mara wameendelea kuadhimisha siku hiyo kwa kutembelea Wodi la Watoto Wachanga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara na kutoa zawadi kwa wazazi waliyojifungua watoto hao.

Katika wodi hilo la watoto wachanga, waandishi wa ahabari wanawake walipata elimu ya namna watoto hao wachanga wanavyotunzwa elimu hiyo ilitolewa na Muuguzi Kiongozi Bi Annastela Ishengoma.