Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

UMOJA WA WANAWAKE WA ASASI ZA KIRAIA WILAYA YA TARIME WATOA ZAWADI KWA KINAMAMA WALIOPO KATIKA WODI YA WAZAZI

Posted on: March 8th, 2024

Ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi, 08 ulimwenguni.

Siku ya Leo Tarehe 09/03/2024 Umoja wa Wanawake wa Asasi za Kiraia kutoka Nyamongo Wilaya ya Tarime Mkoani Mara wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara na kutoa zawadi mbalimbali katika Wodi ya Wazazi.

Bi Emiliana ambaye ni kiongozi wa Msafara huo alisema kuwa wao walitenga mwezi huu kuwa ni mwezi wa wanawake ambao walianza kuadhimisha kuanzia tarehe 01/03/2024 hadi tarehe 17/03/2024.

Pia aliongezea kuwa katika maadhimisho haya waliandaa programu mbalimbali ambapo moja ya programu ilikuwa ni kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara na kuwafariji wagonjwa lakini pia kutoa zawadi mbalimbali.

Aidha, Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt Osimund Dyegura ameshukuru umoja huo wa wanawake wa Asasi za Kiraia kutenga muda wao na kuja kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa lengo la kuwafariji wagonjwa na kuwataka kila wanapopata nafasi waweze kuja kutembelea wagonjwa.

Umoja huo wa Wanawake wa Asasi za Kiraia kutoka Nyamongo Wilaya ya Tarime ulikuwa ni umoja wa Asasi mbili ambazo ziliungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambazo ni Health and Safe delivery baby Foundation (HSF) pamoja na Shirika la Power Life Health and Wealth Solution.