Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

MATUKIO KATIKA PICHA

Posted on: July 9th, 2024

Wizara ya afya ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali Pathfinder wanaosimamia mradi wa M-MAMA wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waratibu wa elimu kwa umma ngazi ya mkoa na halmashauri pamoja na maafisa habari wa Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kuhusu uratibu wa mfumo wa M-mama.

Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika ukumbi wa John Rudin Manispaa ya Musoma tarehe 08/07/2024 yenye lengo la kwenda kutoa elimu katika jamii kuhusu huduma ya dharura ya M-mama na matumizi ya namba 115 endapo mama mjamzito atapata dharura kama kutoka damu sehemu za siri, kutoa maji sehemu za siri, kuumwa kichwa ili kuweza kupata usafiri wa kumuwaisha katika kituo cha afya kilichopo jirani kwa kutumia madereva jamii waliosajiliwa kupitia M-MAMA.

Pia katika mafunzo hayo uliandaliwa mpango kazi wa kufundishia viongozi na wataalam ngazi ya jamii juu ya mfumo wa M-MAMA ili kuongeza uelewa kwa jamii umuhimu wa kutumia vituo vya afya kwa wakati na matumizi ya namba 115.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu.