MASHINE YA KISASA YA MIONZI 9DIGITAL X-RAY)YAANZA KUFANYA KAZI
Posted on: June 7th, 2020MASHINE YA KISASA YA MIONZI (Digital x-ray) YAANZA KUFANYA KAZI
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara imeanza kutoa huduma za kisasa za uchunguzi wa mionzi kwa kutumia mashine ya kisasa (Digital x-ray machine) iliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto ikiwa ni mkakati wa kuboresha huduma za afya katika hospitali za rufaa za Mikoa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo,kaimu Mganga Mfawidhi Dr.Lazaro Mwikwabe ameishukuru serikali ya awamu ya tano kuona umuhimu wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwa kuleta vifaa tiba vya kisasa ili kusaidia upatikanaji wa huduma bora.
Sambamba na hilo Dr.Mwikwabe amewakaribisha wananchi wa Mkoa wa Mara kufika katika hospitali ya rufaa ili kupata huduma bora za matibabu na vipimo ikiwemo huduma ya uchunguzi wa mionzi.
Kwa upande wake mtaalamu wa mionzi katika Hospitali ya rufaa bwn.Hussein Mohammed amesema mtambo huu wa kisasa utasaidia kutoa huduma nzuri kwa jamii kwa sababu una uwezo wa kuhudumia wagonjwa wengi kwa muda mfupi na kutoa picha bora.
Aidha ameahidi kushirikiana vyema na wataalamu wenzake katika kutoa huduma zilizo bora kwa wagonjwa pamoja na kuhimiza kuitunza mashine hii ili idumu katika ubora wake kwa muda mrefu na wananchi waendelee kupata huduma