Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

MAFUNZO YA NAMNA YA KUZUIA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZI MAHALA PA KAZI NA KWENYE JAMII INAYOTUZUNGUKA (IPC)

Posted on: April 7th, 2024

Siku ya leo tarehe 08/04/2024 yameendeshwa mafunzo ya namna ya kuzuia na kudhibiti maambukizi mahala pa kazi na kwenye jamii inayotuzunguka (IPC) kwa watumishi 22 wa kitengo cha usafi.

Lengo kubwa la mafunzo haya ni kujanga uwelewa wa pamoja kuhusiana na shughuli za kuzuia na kudhibiti maambukizi mahala pa kazi na kwenye jamii inayotuzunguka na kuhakikisha usalama wa mteja na mtoa huduma umezingatiwa na kuzuia maambukizi yatokanayo na huduma za Afya (Health Core Associated Infections).

Mafunzo haya yameratibiwa na kitengo cha ubora wa huduma (QIT-Quality Improvement Team) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara.