Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

MADAKTARI BIGWA WAWASILI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA KWA HUDUMA YA SIKU TANO.

Posted on: February 16th, 2020

Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Upasuaji,Moyo,Mishipa ya fahamu,Magonjwa ya akina mama,Pua,Koo na Masikio Pamoja na magonjwa ya mifupa na viungo wamewasili leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Mara na maeneo jirani.

Huduma hizi zinatarajia kuanza kutolewa kesho tarehe 24/2/2020 hadi 28/2/2020 kuanzia saa 2:00 asubuhi na Madaktari Bigwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara wakishirikiana na Madaktari bigwa kutoka India,Hospitali ya Taifa Muhimbili,Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Mnazi Mmoja-zanzibar,hospitali yaTemeke, Tumbi pamoja na Hubert Kairuki Memorial University (HKMU).

Baada ya kuwasili Madaktari hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali ikiwemo jengo la Maabara, ICU, OPD na vyumba vya Upasuaji (Theaters) na kufurahishwa na namna ambavyo Hospitali ya rufaaa ya mkoa wa Mara ina vifaa  vya kisasa vya kutolea huduma jambo ambalo wamesema limewapa nguvu na ari ya kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa.

Pia wametoa pongezi kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa(Mwalimu Nyerere Memorial Medical Center)ambayo Ujenzi wake unaenda kwa kasi kubwa.

Sambamba na hilo wamelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa  kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kuhakikisha ujenzi wa Hospitali Hiyo unakuwa wa ufanisi wa hali ya juu na unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu katika hospitali yao waliyoisubiri kwa muda mrefu ikamilike.

Kwa upande wao wananchi wa Mkoa wa Mara wameishukuru serikali pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara kuamua kuwasogezea huduma hizi muhimu karibu na kutoa ombi kuwa huduma kama hizi zifanyike Mara kwa Mara ili kuwasaidia wananchi na kuwapunguzia gharama wanazozipata kwa kufuata huduma hizi muhimu mbali.