Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

HITIMISHO LA MAFUNZO YA 5S KAIZEN

Posted on: March 27th, 2024

Mafunzo ya 5S KAIZEN yamehitimishwa siku ya leo ya Machi 28, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara.

Mafunzo yalitolewa kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara ambapo yalichukuwa siku nne kuanzia tarehe 25/03/2024 na kukamilika tarehe ya leo 28/03/2024 na watoa mafunzo walitoka katika idara ya ubora (QIT) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara.

Akifunga Mafunzo hayo Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Mara Dkt, Elias Godfrey alishauri kuwa mafunzo waliyopata watumishi yatumike kuwaongezea alama (CPD Point) ili kuwawezesha kuhuisha leseni zao.

Pia aliongezea kuwa umuhimu wa watumishi kutumia elimu waliyopata kuboresha maeneo ya huduma ili kuongeza usalama na ufanisi kwa watumishi na wateja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo Bw. Venance Bwire amesema kuwa mafunzo haya yatakuwa chahcu na kuamsha morali kwa watumishi kwenda kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi.

Mafunzo haya ya 5S KAIZEN ni mafunzo ambayo yanamsaidia mtoa huduma kuandaa eneo lake la kazi ili aweze kutoa huduma bora ikiwa na kumjengea uwezo mtoa huduma kutatua matatizo mbalimbali kwenye eneo lake ili aweze kuboresha huduma kwa wateja ikiwemo na kumuhudumia mteja kwa wakati.