Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

HOSPITALI YA MWALIM NYERERE YAJENGWA KWA KASI

Posted on: October 18th, 2019

Hospitali ya Mwalimu Nyerere iliyoanza kujengwa Toka enzi za Utawala wa Baba wa taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere inamaliziwa kwa kasi kwa usimamizi wa Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt John joseph Pombe Magufuli kupitia WIzara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto ikiwa ni juhudi za kuendeleza Ndoto ya Mwalim Nyerere ambayo ilikua bado haijatimia.

Akizungumza wakati alipotembelea jingo la Hospitali hiyo katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula amesema kua serikali imeshamlipa mkandarasi ambae ni Shirika la Nyumba la Taifa NHC Zaidi ya Billioni 4 na nimatarajio yake hospitali hiyo itaisha ndani ya muda wa mkataba kwakua inajengwa kwa kasi sana.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dr Grace Magembe amesema kua timu kutoka wizarani ilifika katika jengo hilo na kwa kushirikiana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara waliandaa tathmini ya mahitaji ya kuweza kulimalizia jengo hilo na kuipeleka serikrilini na kwa kuanzia serikali ikatoa Zaidi ya Bilioni 4 ya Ngwe ya kwanza inayotarajiwa kuisha mwezi wa kwanza kati ya Bilioni 15.8 za mradi mzima. Aidha ameongeza kua kukamilika kwa hospiatali hii kutapunguza adha ya wananchi wa mkoa wa mara, mikoa jirani na nchi za jirani kwenda mbali kupata huduma za kibingwa lakini pia mkoa utaongeza mapato kupitia Utalii wa kimatibabu (Medical Tourism) hasa kutoka nchi jirani.

Kwa upande wake nae pia Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa mara Dr Joachim Eyembe ametoa Shukrani kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Uongozi Mzima wa Wizara ya Afya kwa kulimalizia jengo hilo na kufuatilia mara kwa mara maendeleo ya ujenzi huo ili kuhakikisha linamalizika kwa wakati.

Hospitali ya Mwalimu Nyerere iliyoanza kujengwa Tokea enzi za Utawala wa Baba wa taifa inamaliziwa kwa kasi kwa usimamizi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John joseph Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto ikiwa ni juhudi za kuendeleza Ndoto ya Mwalimu Nyerere ambayo ilikua bado haijatimia.

Akizungumza wakati alipotembelea Hospitali hiyo katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula amesema serikali imeshamlipa mkandarasi ambae ni shilika la nyumba la taifa (NHC) Billioni 4.5 na nimatarajio yake hospitali itaisha ndani ya muda wa mkataba kwakua inajengwa kwa kasi sana.

Tazama Hapa>>>