Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

HABARI PICHA

Posted on: June 26th, 2024

Chama cha Wanawake (Dorikasi) kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato kata ya Kamunyonge-Manispaa ya Musoma siku ya leo tarehe Juni 27, 2024 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa lengo la kuwajulia hali wagonjwa na kutoa majitoleo mbalimbali katika wodi ya wazazi, watoto wachanga pamoja na wodi ya watoto kuanzia mwezi mmoja na kuendelea.


Dr. Nelly M Jackson ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuwapokea na kutoa majitoleo hayo, pia ameongezea wataenda kuwa mabalozi wazuri kupitia elimu ya namna ya kujikinga na kipindupindu.


Chama cha Wanawake (Dorikasi) kimetoa matunda, vitenge, mafuta pamoja na sabuni katika wodi ya wazazi, watoto wachanga pamoja na wodi ya watoto kuanzia mwezi mmoja na kuendelea.