Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

ELIMU YA SICKLE CELL (SELI MUNDU) YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WANAOISHI NA UGONJWA WA SICKLE CELL (SELI MUNDU)

Posted on: April 17th, 2024


Siku ya leo tarehe 17/04/2024 wazazi wenye watoto wanaoishi na changamoto ya ugonjwa wa Sickle Cell (SeliMundu) wamepata elimu ya chanzo na dalili za ugonjwa huo.Pia wazazi hao walielezwa umuhimu wa watoto kuhudhuria kliniki ya Sickle cell.

Elimu hiyo ilitolewa katika Shule ya Msingi ya Mkendo iliyoko Manispaa ya Musoma, Pia wazazi walihamasishwa kujiunga na Bima ya Afya ili kupunguza gharama za matibabu.

Mmoja wa wazazi waliyopata elimu hiyo alishukuru na kuomba elimu hiyo hiwe endelevu kwa shule nyingine ili wazazi wengi wawe na uelewa kuhusu ugonjwa wa Sickle Cell (SeliMundu).

Zoezi hili la utoaji elimu limeratibiwa na Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Bi. Esther Muya kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Mratibu kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Mkoa wa Mara.