Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

ELIMU YA AFYA KUHUSU MGUU KIFUNDO YATOLEWA KWA WANANCHI WALIYOFIKA MNMRRH - MARA KWA AJILI YA MATIBABU

Posted on: February 14th, 2024

Kitengo cha Fiziotherapi siku ya leo tarehe 15/02/2024 wametoa elimu ya afya kuhusu Mguu kifundo kwa wananchi waliyofika Hosipitali kwa ajili ya matibabu.


Elimu ya Mguu kifundo ilijikita katika maeneo tofauti tofauti na miongoni mwa maeneo waliyogusia ni kama vile maana ya mguu kifundo, visababishi vya mguu kifundo, madhara yake na hatua mbalimbali za matibabu.


Elimu hii imetolewa na Wilson Mzungu Afisa Fiziotherapia, Omary Majuara Afisa Fiziotherapia, Godwill Kimaro Fiziotherapia pamoja na Catherine Urio Fiziotherapia kutoka kitengo cha Fiziotherapi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.


Matibabu haya ya Mguu kifundo yanatolewa hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere chini ya ufadhili wa taasisi ya MDH (Management and Development for Health) kwa Watoto chini ya miaka mitano.


Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii kupata elimu hii ya mguu kifundo kwa njia ya video.