CHANGAMOTO MBALIMBALI ZAJADILIWA KATI YA UONGOZI WA HOSPITALI PAMOJA NA MADEREVA WA PIKIPIKI (BODABODA) WANAOPAKI NDANI YA HOSPITALI
Posted on: February 13th, 2024Siku ya jana tarehe 13/02/2024 uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Mara ukiongozwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Elias Godfrey waliendesha kikao pamoja na madereva pikipiki (bodaboda) wanaopaki ndani ya Hospitali.
Kikao hicho kililenga kujadili Changamoto mbalimbali zinazoripotiwa na wananchi wanaofika kwa ajili ya kupatiwa matibabu na watumishi likiwemo la kupandisha nauli kiholela, kutokuwa na lugha nzuri kwa wateja, pia kutokuwa na sare za kazi.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Elias Godfrey aliwataka madereva hao wa pikipiki (bodaboda) kuwa na lugha nzuri na kuwajali wateja wanaowahudumia kwa kutopandisha nauli kiholela na kuweka bei rafiki kwa wateja wao.
Pia aliwataka madereva hao wa pikipiki (bodaboda) kuwa na vitambulisho au reflector ambazo zitawatambulisha kuwa wanapaki eneo la Hospitali ili kulinda usalama wao na wateja wanaowahudumia kwani kuna muda wanakuja bodaboda wengine wanapaki hapa na siku wakifanya uhalifu itakuwa ngumu kuwatofautisha.