Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

BIMA YA AFYA NDIO MFUMO BORA, RAHISI NA ENDELEVU.

Posted on: November 1st, 2023

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, leo Bungeni Jijini Dodoma amewasilisha muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa Mwaka 2022, amesema kuwa Bima ya afya ndio mfumo bora, rahisi na endelevu ambao umethibitika katika nchi mbalimbali duniani kuwawezesha wananchi wengi hususani wa kipato cha chini kupata huduma bora za Afya pindi wanapohitaji.