Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

UJIO WA MADAKTARI BINGWA WA MACHO

TANGAZO

TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kumbukumbuku ya Mwalimu J.K Nyerere, inapenda kuwatangazia wananchi wote ujio wa Madaktari Bingwa wa Macho kuanzia tarehe 20/11/2023 hadi tarehe 24/11/2023. Huduma hiyo itatolewa na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Kanda ya Bugando Kwa kushirikiana na Madaktari waliopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 10:00 jioni.

Wateja walio na kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ASSEMBLE INSURANCE, STRATEGIES, NSSF NA TPDF zitapokelewa.

Aidha kwa wateja wasiokuwa na Bima yoyote watalipia kulingana na utaratibu wa malipo wa siku zote wa Hospitali.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Osimund Dyegura

MGANGA MFAWIDHI

10/11/2023

- 11 November 2023