Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA MNMRRH KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA SERENGETI KIBEYO

Posted on: June 9th, 2026

Madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Madaktari wa hospitali ya wilaya ya Serengeti wameweka kambi ya kutoa huduma za kibingwa katika hospitali ya wilaya ya Serengeti Kibeyo ambapo huduma mbalimbali za kibingwa zinatolewa.

Kambi hiyo ya madaktari Bingwa inafanyika kwa siku tano mfululizo ambapo imeanza rasmi tarehe 8/06/2026 na kukamilika 12/06/2026 ambapo huduma za kiningwa zinatolewa kama vile, Magonjwa ya Watoto, Magonjwa ya Ndani, Huduma za upasuaji, Magonjwa ya Mifupa, Huduma za Radiolojia (MIONZI), Magonjwa ya macho, Huduma ya Masikio, Pua na Koo, Huduma ya usingizi Tiba na Ganzi salama, Huduma za Dharura, Magonjwa ya wanawake na uzazi, Mtaalam wa Utengemao.

Aidha mbali na huduma hizo za kibingwa kusogezwa kwa wananchi wa Serengeti, Watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Serengeti pia wamepata nafasi ya kujengewa uwezo kutoka kwa Madakatri bingwa katika kambi hiyo