Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

MAADHIMISHO YA SARATANI YA MACHO KWA WATOTO (RETINOBLASTOMA)

Ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, inapenda kuwataarifu kuhusu wiki ya maadhimisho ya saratani ya macho kwa watoto itakayoanza tarehe 11/6/2026 hadi 15/6/2026 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 9:30 alasiri.

Huduma zitakazotolewa;

Elimu ya saratani ya macho kwa Watoto

Uchunguzi wa Saratani ya macho

Uchunguzi wa mtoto wa jicho

Kupima presha ya macho

Uchunguzi wa mzio

Hivyo wote wenye matatizo na wanaohitaji huduma wafike katika uwanja wa Mukendo, Manispaa ya Musoma  ili waweze kupata huduma hizo muhimu. Huduma hizi zitatolewa bure.

- 05 May 2026