Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

MAFINDOFINDO

Posted on: October 17th, 2019

UFAHAMU NA ELIMU YA UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS)
-
Tonsils au Mafindofindo ni maambukizi yanayojitokeza katika viungo viwili vidogo vinavyopatikana nyuma ya koo. Sehemu hizi huwa ni mojawapo ya viungo vya mwili vinavyohusika na ulinzi, yaani kuharibu vijidudu vinavyosababisha magonjwa
-
Ikitokea kasi na nguvu ya wadudu hawa imekuwa kubwa sana viungo hivi huzidiwa nguvu na vinaposhindwa kufanya kazi lymph huvimba na husababisha ugonjwa kutokea
-
Dalili zake huambatana na Maumivu ya koo, kuvimba kwa tonsils, maumivu wakati wa kufungua kinywa, ugumu katika kumeza mate/chakula, homa, kuvimba kwa Lymph Nodes kwenye shingo, kukakamaa kwa shingo na maumivu ya tumbo hasa kwa watoto wadogo
-
Ukienda hospitalini utapatiwa tiba lakini tiba unayoweza kujipatia mwenyewe ni kunywa maji ya uvuguvugu kila mara (angalau mara 4 kwa siku) yenye chumvi kiasi, asali pamoja na ndimu/limao