Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

UHAKIKI WA UTAFITI ULIYOFANYWA NA CHUO CHA USTAWI WA JAMII DAR ES SALAAM.

Posted on: November 6th, 2023

Siku ya tarehe 24 ya mwezi wa 10/2023, Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere kulifanyika uhakiki wa ripoti ya utafiti uliyofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo Dar es salaam kuhusu Mila na Desturi zinazomlinda Mwanamke dhidi ya ukatili wa kijinsia. Ripoti hiyo iliwasilishwa na Dkt. William Manyama Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es salam. Utafiti huo umefanywa kuanzia mwaka 2022 huku ukihusisha mikoa ya Mara, Tanga na Mbeya. Kwa mujibu wa Dkt. William Manyama Mhadhiri Mwandamizi alisema kuwa utafiti huo umelenga Wazee kwasababu ya uzoefu na ndiyo kundi linalojua zaidi mila na desturi.