MGODI WA NORTH MARA WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA
Posted on: August 17th, 2021Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara Leo Agosti 18 2021 imepokea msaada waVifaa tiba mbalimbali kutoka kikundi cha wafanyakazi wa Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa North Mara kinachoitwa Kijiwemuso.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Vifaa hivyo Daktari kiongozi wa Mgodi Huo dkt. Robert Mazengo amesema kuwa dhumuni la kutoa vifaa hivyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha huduma za Afya nchini.
“Tumeamua kutoa vifaa hivi ili viweze kusaidia jamii ya watanzani wenzetu ambao wapo kwenye changamoto ya upumuaji kipindi hiki cha janga la UVIKO 19 na nipende kutoa wito kwa watumishi kutumia vifaa hivi kwa uthabiti ili viweze kuokoa maisha ya watanzani.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,dkt. Lazaro Mwikwabe amewashukuru watumishi hao kwa weledi wao kuunga mkono juhudi za serikali na kuona umuhimu wa kusaidia wananchi wengine ambao wana uhitaji hususani katika wakati huu ambapo vifaa hivi vinahitajika sana ili kuokoa maisha ya watanzania wanaosumbuliwa na ugonjwa wa UVIKO 19.
“Mimi nimejifunza na watanzania wengine wajifunze kuwa kumbe kuna watu katika vikundi vya jamii wanaweza kujinyima na kutumia kiasi kidogo walichonacho kwenye akiba zao kuweza kusaidia na kujali watu wengine”.
Aidha amewaasa wafanyakazi katika sehemu mbalimbali watambue kuwa wana wajibu wa kurudisha faida wanayoipata kwa jamii inayowazunguka hivyo kiasi kidogo ambacho wanaweza kuona hakifai kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa wahitaji.
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vifaa vya kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji {Ventilator,Thermoscanner,paxocimiter,nasal proms na gloves}pamoja na vifaa vitakavyosaidia Akina Mama kufunga vitovu vya watoto wachanga baada ya kujifungua.