Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

KIKAO KAZI CHA MABORESHO YA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

Posted on: November 17th, 2023

Katika kuendelea kuimarisha utoaji huduma bora za matibabu kwa wananchi, siku ya Tarehe 16/11/2023 timu ya maboresho (QIT) ilifanya kikao kwa lengo la kuibua changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utoaji huduma za afya kwa wananchi na namna kutatua changamoto hizo maeneo mbalimbali ya taasisi.