Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

KATIBU TAWALA WA MKOA WA MARA AMEWASIHI WATUMISHI KUWA NA LUGHA NZURI KWA WAGONJWA.

Posted on: December 7th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Mhe. Msalika Makungu ametembelea hospital ya kumbukumbu ya mwalimu nyerere na kuongea na watumishi wa hopital hiyo. Richa ya kuridhishwa na huduma zinazitolewa amewasihi watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kutumia lugha nzuri pale wanapokuwa wanahudumia wateja.


Amezungumza hayo akiwa katika ziara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya jana tarehe 06/12/2023 kuangalia utekelezaji wa huduma mbalimbali za Hospitali.


Katibu Tawala amewaomba pia watumishi kuwa makini katika mazungumzo yao na kuangalia wanazungumza na nani kwa mda huo kwa maana kuwa wao ndo wana taarifa za wateja wanaowahudumia.