Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

HUDUMA YA UPIMAJI MAGONJWA YASIYOKUWA YA KUAMBUKIZWA IMETOLEWA KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MARA

Posted on: November 7th, 2023

Siku ya tarehe 26/10/2023, Huduma ya upimaji wa Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ilitolewa katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Zoezi la upimaji Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza iliambatana na upimaji macho pamoja na upimaji wa virusi vya ukimwi kutoka kwa watoa huduma na Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere, Huduma hiyo ilihusisha watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Taasisi na Mashirika mbalimbali ya kiserikali pamoja na wananchi mbalimbali waliyokuwa eneo hilo.

Huduma zilizokuwa zikitolewa zilikuwa ni kama ifuatavyo:
1) Upimaji wa kisukari
2) Shinikizo la Damu
3) Urefu na uzito
4) Ushauri
5) Upimaji Macho
6) Upimaji wa virusi vya ukimwi