HOSPITALI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUJIANDAA NA HUDUMA ZA DHARURA
Posted on: November 30th, 2023Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Hospitali zote nchini kujiandaa kutoa huduma za dharura na ajali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa Mwaka.
Waziri Ummy amesema hayo jana Novemba 29, 2023 akitoa taarifa ya mpango wa Rais Samia wa kuongeza wataalamu bingwa na bobezi wa Afya wataki akiongea na waandishi na habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salam.
“Tunapenda ajali zisitokee lakini tunaanza kwanza kutoa wito kwa wataalamu wa Afya ili kujiandaa kwa kuwa ajali zinatokea katika maeneo mbalimbali nchini.” Amesema Waziri Ummy
Pia, ametoa wito kwa Watanzania kuendesha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika.