Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YAKABIDHIWA MAGARI MAWILI

Posted on: December 3rd, 2023

HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YAKABIDHIWA MAGARI MAWILI


Katibu tawala wa Mkoa wa Mara mhe. Msalika Makungu siku ya tarehe 02/12/2023 alikabidhi magari mawili Moja likiwa la kubebea wagonjwa na lingine la usimamizi shirikishi kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dkt Osimund Dyegura kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.


Magari hayo ya kubebea wagonjwa pamoja na usimamizi shirikishi yaliyokabidhiwa yalizinduliwa siku ya tarehe 28/10/2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassani katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam.


Jumla ya magari yalikuwa 989 ambayo yalitolewa nchi nzima na kwa Mkoa wa Mara ulikabidhiwa magari 31 ikiwemo ambulance 20.