HABARI PICHA
Posted on: July 27th, 2024Katika kuendelea kutoa huduma bora za maabara kwa wananchi wa Mkoa wa Mara na maeneo jirani tarehe 26 Julai, 2024 idara ya Maabara ikishirikiana na menejiment ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ilifanya kikao cha mapitio ya uendeshaji wa huduma za maabara.
Katika kikao hicho idara ya Maabara ikiongozwa na Mkuu wa idara Bw. Kenendy Fussy iliezea hali halisi ya uhai wa maabara katika kutoa huduma yaani vitendea kazi kama vile mashine, vitendanishi na uwepo wa wafanya kazi wanaoweza kutosheleza kutoa huduma hiyo.
Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika kikao hicho iliongozwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Osimund Dyegura.