Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

UJIO WA MADAKTARI BINGWA KUANZIA TAREHE 23/2/2020 HADI TAREHE 28/2/2020

Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara wakishirikiana na Madaktari bingwa kutoka India na Hospitali ya Taifa Muhimbili wanatarajia kutoa huduma za matibabu ya Magonjwa ya Upasuaji(general surgery), Magonjwa ya pua,koo na masikio(ENT), Magonjwa ya  Moyo(cardiologist), Magonjwa ya ndani(internal medicine), Magonjwa ya upasuaji wa mifupa(orthopedic) pamoja na Magonjwa ya upasuaji wa mishipa ya fahamu(neuro surgery) .Huduma hii itafanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12jioni Hivyo wananchi wote wa Mkoa wa Mara na maeneo Jirani mnakaribishwa kupata hudumu hizo muhimu. 

Pia huduma za wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), AAR na NSSF zitatolewa.

- 18 February 2020