TANGAZO LA NAFASI YA UWAKILISHI WA UJUMBE WA BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA.
MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MARA WENYE MAPENZI MEMA NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA, KUOMBA NAFASI YA UWAKILISHI WA WAJUMBE WA BODI YA USHAURI YA HOSPITALI.
WAOMBAJI WATATAKIWA KUWA NA SIFA ZIFUATAZO:
1. Wawakilishi kutoka sekta binafsi (3)
2. Mwanasheria/Wakili (2)
3. Mstaafu katika sekta ya Afya/ ustawi wa Jamii (3)
4. Wawakilishi kutoka ushirika/umoja wa wanawake (3)
5. Wawakilishi kutoka mashirika ya dini (FBOs) (2)
6. Wataalamu wa masuala ya fedha (3)
7. Wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi (3)
8. Wawakilishi kutoka ngazi yaHalmashauri / Wilaya (3)
9. Wawakilishi kutoka kituo cha afya kilichopo karibu na hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara (3)
10. Wawakilishi wa watumiaji wa huduma (2)
N.B
Wote ambao wanasifa tajwa hapo juu,watatakiwa kutuma maombi yaliombatana na wasifu kulingana na nafasi husika, kwa kutumia anuani zifuatazo.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, S.L.P 21, Musoma au barua pepe,musomarrh@afya.go.tz au fika moja kwa moja ofisi ya Mganga Mfawidhi wa hospitali, mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 1/06/2021.
Tangazo la nafasi ya uwakilishi wa bodi ya ushauri wa hospitali ya mkoa wa mara.pdf